Exodus 7:1-2

1 aKisha Bwana akamwambia Musa, “Tazama, nimekufanya kuwa kama Mungu kwa Farao, naye Haruni, huyo ndugu yako, atakuwa nabii wako. 2Utasema kila kitu nitakachokuagiza, naye Haruni ndugu yako atamwambia Farao awaachie Waisraeli watoke katika nchi yake.
Copyright information for SwhKC